Kijana mmoja aitwae Shazili Saidi Mkuchi
mkazi wa Mtwara mwenye umri wa miaka 26, anatafutwa na polisi kwa
tuhuma za kumuua mama yake mzazi Bi. Amina Chuwalila kwa kumkata na
panga.
Akiongea na mwandishi wa habari kaka wa
mtuhumiwa ambaye pia ni mtoto mkubwa wa marehemu anayejulikana kwa jina
la Rashidi Saidi Mkuchi, amesema mdogo wake huyo amefanya tukio hilo
baada ya kuambiwa na mganga wa kienyeji kuwa mama yake na kaka yake
ndiye anayemroga, na kuamua kumfuata shambani alikokuwa na kumfanyia
tukio hilo, ambalo limekatisha uhai wake.
“Kama angemkosa mama, basi kifo hiki
kingekuwa cha kwangu maana na mimi nimetajwa kuwa nilikuwa nashirikiana
na mama yetu kumroga yeye”, amesema kaka wa mtuhumiwa Saidi.
Daktari wa kituo cha afya cha Nanguruwe
aliyejulikana kwa jina la Dokta Adam amekiri kumpokea mama huyo akiwa
amejeruhiwa vibaya, na kwamba tayari alikuwa ameshafariki.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Lucas
Mkondya amethibitisha kuripotiwa kwa tukio hilo ambalo limetokea Machi
14, na kuwataka wananchi kusaidia kufanikisha kumpata mtuhumiwa huyo
ambaye ametokomea kusikojulikana.
Marehem alipokelewa na Dokta Adam wa
Kituo cha Afya Nanguruwe na kuthibitisha kuwa alifika Kituoni hapo akiwa
tayari Ameshaaga Dunia.
No comments:
Post a Comment