Mwalimu wa shule ya sekondari ya
Nyakisasa iliyopo mkoani Kagera anayetambulika kwa majina ya Deogratias
Simon anashikiliwa na jeshi la polisi Kagera kwa tuhuma za kumkashfu
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera
Augustine Ollom amesema kuwa mwalimu huyo anashikiliwa kwa kosa la
kutumia ukurasa wake wa Facebook kuikashfu serikali na kumkashfu Rais
Magufuli kuwa ni Dikteta na anaminya demokrasia.
Aidha amesema kuwa kufutia hali hiyo
tayari yupo mikononi mwa polisi na watakwenda naye mpaka dakika ya
mwisho ili sheria iweze kutenda haki huku Kamanda amewaomba wananchi
kuendelea kufichua watu wenye vitendo vya namna hiyo ili wawakabidhi
polisi ili washughulikiwe
No comments:
Post a Comment