Arusha

Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre—ALMC—chini ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, imeweka historia mpya katika safari ya kuboresha huduma kwa watoto njiti na wale wanaozaliwa kabla ya muda kwa kuingia makubaliano  na ICHA taasisi ya Mtoto Africa ili kuendeleza na kuboresha huduma hiyo ndani ya hospital hiyo.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo Mkurugenzi mtendaji wa hospital ya ALMC MKOANI Arusha Godwill Kivuyo amesema huduma hii itasaidi kila mtoto anaye zaliwa kupata nafasi ya kuishi hata kama atazaliwa kabla ya Muda wake.

“Ushirikiano huu mpya kati ya ALMC na ICHA—Taasisi ya Afya ya Mtoto Afrika kutoka Marekani—unafungua ukurasa mpya wa matumaini. Tunataka kuhakikisha kila mtoto anayejaaliwa kuzaliwa hapa, awe na nafasi bora ya kuishi na kukua katika mazingira salama.”

Daktari Stephen Swanson ni Mratibu wa Taasisi ya mtoto Africa (ICHA) amesema Kwa muda mrefu, changamoto za vifaa, wataalamu na teknolojia ya kisasa zimekuwa kikwazo kwa vitengo vya watoto njiti katika hospitali nyingi za Tanzania Lakini kupitia makubaliano haya mapya, safari ya mabadiliko imeanza rasmi.

“ICHA inajivunia kushirikiana na ALMC kwa sababu tunaamini katika uwezo wao. Lengo letu ni kuleta utaalamu, mafunzo, na vifaa vinavyoweza kubadilisha kabisa huduma za neonatal. Watoto hawa ni wadogo, lakini matumaini yao ni makubwa.”

Aidha Daktari wa watoto Dkt. Eunice Msuya  ambaye amekuwa akihusika na watoto njiti katika hospital hiyo amebainisha namna ambavyo ushirikiano huo unatarajiwa kuwa kitovu cha huduma za kiwango cha juu, si tu kwa Arusha bali kwa Kanda nzima ya Kaskazini na Africa.

“Hawa ni watoto wanaohitaji uangalizi wa karibu, ujuzi wa hali ya juu, na vifaa mahususi. Usimamizi sahihi katika dakika na saa za kwanza baada ya kuzaliwa huamua maisha yao. Tuna shukrani kubwa kwa programu hii ambayo itaongeza uwezo wetu wa kutibu na kuokoa maisha Wengi zaidi.”

Utafiti wa “Neonatal and Infant Mortality Risk” nchini Tanzania ulionesha kuwa watoto ambao wamezaliwa kabla ya muda wana hatari kubwa ya kifo  kwani wanaweza kukabiliana na matatizo kama  kupumua, kuzuia baridi , maambukizi, na shida za kukua baadaye hatua hii mpya ya ALMC na ICHA wanaandika hadithi ya matumaini hadithi ya ushirikiano  itakayo saidia kupunguza Vifo vya watoto Njiti.

AFYA: MAKUBALIANO YA (ALMC) HOSPITAL ARUSHA NA (ICHA) KUBORESHA HUDUMA ZA MTOTO NJITI TANZANIA NA AFRICA KWA UJUMLA

No comments:

Post a Comment