MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jana ilisema itatoa uamuzi wa maombi ya
dhamana ya mfanyabiashara Audai Ismail (43) na wenzake saba
wanaokabiliwa kesi ya uhujumu uchumi, ikiwamo kujiunganisha bomba la
mafuta aina ya dizeli mali ya Mamlaka ya Bandari (TPA), Aprili 5, mwaka
huu.
Jana kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kusikilizwa uamuzi wa dhamana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Wakili wa serikali, Elia Atanas alidai kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kusikilizwa uamuzi wa maombi ya dhamana, Hakimu alisema uamuzi wa maombi hayo bado haujawa tayari na kwamba utasomwa Aprili 5.
Mbali na Ismail washtakiwa wengine ni aliyekua mfanyakazi Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia(TAZAMA) Samwel Nyakirang'ani (63), mwalimu wa Shule ya Msingi Ufukoni, Nyangi Mataro (54), Farijia Ahmed (39), Malaki Mathias (39), Kristomsi Angelus (25), fundi ujenzi Pamfili Nkoronko (40) na Henry Fredrick (38).
Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, mwaka huu katika eneo la Tungi Muungano, wilaya ya Kigamboni, washtakiwa kwa pamoja walijiunganishia bomba la mafuta ya dizeli lenye upana wa inchi moja kutoka katika bomba lenye upana wa inchi 24, bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Bandari (TPA).
Ilidaiwa kuwa walijiunganishia mafuta hayo kutoka katika bomba rangi ya silva lenye upana wa inchi 24 ambalo halishiki kutu.
Shitaka jingine ni kuharibu miundombinu inayotumika kutoa huduma muhimu, ambapo wanadaiwa katika kipindi hicho na kwenye eneo hilo walitoboa na kuharibu bomba la mafuta ya dizeli lenye upana wa inchi 24, ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta mali ya Mamlaka ya Bandari (TPA).
Pia wanadaiwa walitoboa na kuharibu bomba la mafuta mazito (crude oil) lenye upana wa inchi 28, ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta ghafi mali ya TPA.
Wakili Athanas alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

No comments:
Post a Comment