Imeelezwa kuwa
migogoro ya kifamilia katika jamii imekuwa ni chanzo kinachosababisha
watoto wadogo kuingia katika makundi mbalimbali yasiyo salama ikiwa ni pamoja
na kuingia katika mahusiano wakiwa na umri mdogo.
Kauli
hiyo imetolewa leo na mtaalamu wa saikolojia ya jamii na mahusiano Bi.
Glory Kasilo wakati akizungumza na Blog hii ambapo amesema kuwa baadhi ya
wazazi katika familia wamekuwa wakichangia kwa kisai kikubwa watoto wadogo
kujiingiza katika mahusiano ya umri mdogo jambo ambalo halikubalki katika jamii
ya kitanzania.
Amesema
kuwa watoto wadogo wanapoona wazazi wao hawako katika mahusiano mazuri wamekuwa
wakijikuta wakiangukia katika mahusiano ya umri mdogo ili kutafuta faraja hali
ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa kwa watoto hao ikiwemo kukatisha
ndoto zao.
Aidha
amewashauri wazazi kuhakikisha wanatekeleza mambo muhimu yanayotakiwa kufanywa
na mzazi huku akiwataka watoto walio chini ya miaka 18 kuacha tabia hiyo kwani
kila kitu huenda kwa wakati hivyo ni vyema wakasubiri wakati utakapofika.
Katika
hatua nyingine Bi Kasilo amesema kuwa amekuwa akukumbana na kesi nyingi akiwa
katika utekelezaji wa majukumu yake zinazohusisha mahusiano ya watoto wadogo
zinazokuwa zikichangiwa na ugumu wa maisha jambo ambalo hupelekea kujikuta
watoto wadogo wakiingia kwenye mahusiano na zaidi ya vijana wa nne kwa lengo la
kujipatia kipato.
No comments:
Post a Comment