media
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewataka viongozi wa dini kuhubiri habari za maendeleo na uchumi wa viwanda kuliko kung’ang’ania masuala aliyosema hayana umuhimu kwa wakati huu nchi ikifikiria kupata maendeleo.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Jumatatu ya wiki hii jijini Dar es Salaam, ambapo alilazmika kugusia suala la viongozi wa dini baada ya maaskofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT kutoa waraka wa Pasaka.
Rais Magufuli amesema “nawashangaa viongozi wetu wa dini wanapigia kelele masuala ambayo hayana msingi na yale yenye msingi na yanayohusu maendeleo ya wananchi wanayaacha.”
Kauli ya rais Magufuli imekuja ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu maaskofu wa kanisa la Kilutheri Tanzania KKKT watoe waraka wa Pasaka ulioubua mjadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu masuala waliyoyajadali kupitia kwenye waraka huo.
“Mimi nadhani sijui tumerogwa, nafikiri tumerogwa hebu tukemee kwa majina yote haya mambo ya ondoke, tukemee kwa jina la Mtume na kwa jina la Yesu Kristo,” alisema rais Magufuli.
Maaskofu hao kwenye waraka wao wameeleza kuguswa na matukio yanayoshuhudiwa hivi sasa nchini Tanzania ya watu kuuawa, kutekwa na majaribio ya mauaji dhidi ya wanasiasa wa upinzani.
Maaskofu hao wametoa wito kwa Serikali kufanya kila linalowezekana kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kusaidia kuondoa hofu ambayo wananchi wengi wanayo kwa sasa kutokana na kuongezeka kwa matukio ambayo wamesema Tanzania haikuyazoea.
Viongozo hao pia waligusia suala la kurejeshwa kwa mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya ambao ulikufa mwaka 2015, wakisema mtu mmoja hawezi kuwa mbadala wa KATIBA MPYA wakiwataka wananchi kuendelea kuzungumza na kushinikiza kurejeshwa kwa mchakato huo.
Mara kadhaa rais Magufulu amenukuliwa na vyombo vya habari nchini humo akisema suala la Katiba mpya sio kipaumbele katika Serikali yake.
Kwenye waraka huo maaskofu pia walieleza kuguswa na namna vyombo vya dola vimekuwa vikitumiwa vibaya kuminya haki za raia na kubanwa kwa uhuru wa watu kutoa maoni yao, wakisema kufanya hivyo kutasababisha wananchi kufikia wakati fulani kuchoka na manyanyaso na kuchukua hatua za kuandamana kudai haki zao.
Katika hotuba yake rais Magufuli amewataka wachungaji na viongozi wengine wa dini kuhubiri amani na yale mambo ya msingi yanayohusu maendeleo na kuwafanya watu kumjua Mungu.

Rais wa Tanzania awataka viongozi wa dini kuhuburi maendeleo na sio vinginevyo

No comments:

Post a Comment