Kasisi mmoja nchini Msumbiji
amejipata mikononi mwa polisi baada ya kujaribu kumfufua mwanamume
mmoja eneo la kati la Msumbiji bila mafanikio.
Kasisi huyo alidai
kuwa roho mtakatifu alimwambia alisafiri hadi katika hospitali ya
Chimoio katika jimbo la Manica, kufanya muujiza huo.
Kasisi huyo
ambaye aliyedai kuwa na uwezo wa kufanya mwujiza huo aliweza kuikonga
mioyo ya maafisa wa hospitali hadi wakamruhusu aingie ndani ya chumba
cha maiti kuutekeleza muujiza wake
Hata hivyo baada ya siku mbili za maombi makali, hakuweza kabisa kurejesha uhai wa marehemu.
Haikuishangaza familia ya marehemu.
Dada yake marehemu - ambaye hakutaka jina lake litajwe - aliwaambia waandishi wa habari:
"Kasisi aliomba, akaomba na kuomba hadi akanena kwa lugha. Alizungusha kichwa cha marehemu huku na kule huku akiomba.
"Lakini
hakuna hata sehemu ya marehemu kaka yangu iliyoweza kutikisika. Wakati
mmoja kasisi alipaza sauti akisema: 'amka, kijana wa Mungu!"
"Hatukuamini
kasisi angefanya mwujiza wowote. Hii ni kwa sababu hakuwahi, hata
wakati mmoja, kuthibitisha uwezo wake wa kumrejeshea mfu uhai wake.
"Tangu wakati huo kasisi alikamatwa na yuko mikononi mwa polisi akishtakiwa kwa kosa la kumkosea heshima mfu."
No comments:
Post a Comment