Hatimaye Hakimu ametoa dhamana kwa washtakiwa Kila mshtakiwa
anatakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini bondi ya Sh. Milioni
20 na wawe na barua toka kwa viongozi wao wa vijiji ama S/Mtaa na wawe
na nakala za vitambulisho vyao.
Maamuzi hayo yametolewa leo na hakimu Wilbrad Mashauri baada ya
kupitia maelezo kutoka pande zote mbili huku akibaini kuwa watuhumiwa
hao walikua na uhalali wa kupata dhamana kwa kuwa makosa yao
yanadhaminika.
Wakili wa Jamhuri anamuomba mkuu wa Logistics za kuleta
wafungwa Kisutu, aliyemtaja kwa jina moja la Shaban aeleze sababu za
watuhumiwa kutofika mahakamani. Shaban anasema asubuhi aliwasiliana na
mkuu wa gereza la Segerea ambaye alisema gari limeharibika.
No comments:
Post a Comment