Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo ametoa zawadi ya vifaa tiba vya Mama mzazi kwaajili ya kujifungulia (Delivery Packs)
200 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi million 20 Kama zawadi yake ya
sikukuu ya pasaka kwa kinamama watakaojifungua kwenye msimu huu wa
pasaka.
Gharama ya mfuko mmoja (package) ya Vifaa hivyo vya kisasa ni
Shilingi laki Moja ambapo ndani yake kuna Mashuka, Vitambaa, Dawa,
Mabomba ya Sindano, Pamba, Kibanio cha kitovu, Nyuzi, pedi za kinamama,
Dawa ya kuzuia upotevu wa damu, Nyembe na Gloves ambapo vitatolewa Bure
kwa Mama mzazi atakaejifungua msimu huu wa pasaka kwenye vituo vya Afya
na zahanati zilizopo kwenye Wilaya Tano za Mkoa huo.
Makonda ametoa vifaa hivyo baada ya kubaini changamoto ya baadhi ya
kinamama kushindwa kumudu gharama ya vifaa vya kujifungulia na kujikuta
wanatumia kanga au nguo jambo ambalo ni hatari kiafya kwa mama na mtoto.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Makonda kwa waganga wakuu wa halmashauri na wasimamizi wa vituo na Zahanati, Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Grace Maghembe amesema vifaa hivyo vitasaidia pia kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
No comments:
Post a Comment