Naye msemaji wa Polisi Kanali Pierrot Mwanamputu amesema ni watu watatu pekee ndio waliopoteza maisha, na kusisitiza kuwa hawakuwa waandamanaji bali watu waliokuwa wanapora mali ya watu.
Aidha, ameongeza kuwa afisa mmoja wa polisi naye aliuawa katika maandamano hayo.
Hii sio mara ya kwanza kwa mvutano kama huu kushuhudiwa wakati kunakuwa na maandamano na kunatokea mauaji katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.
Umoja wa Mataifa, umeitaka serikali ya Kinshasa kuheshimu haki ya kuandamana kwa amani kwa raia wa nchi hiyo.
Mashahidi wanasema watu zaidi ya 140 wakiwemo makasisi walikamatwa na wanaendelea kuzuiliwa katika sehemu mbalimbali nchini DRC.
Huduma
ya mtandao wa Internet na SMS imerejea hatua kwa hatua kuanzia jana
Jumatatu saa tano usiku (saa za Kinshasa), ambapo wananchi wa taifa hilo
tayari wameanza kutumia huduma hiyo iliokatwa tangu siku ya Jumamosi
Usiku.
Waziri wa mawasiliano na uchukuzi Emery
Okundji amesema serikali ya DR Congo iliyataka mashirika yote yanayotoa
huduma hiyo kusitisha huduma hiyo kwa muda, hadi pale watapoamriwa tena
kutokana na sababu za usalama wa taifa.
No comments:
Post a Comment