Wabakaji wa watoto wanapaswa kuuawa
katika muda wa miezi sita tangu watekeleza uovu huo, mteteaji mkuu wa
haki za wanawake India amependekeza.
Swati Maliwal ametoa ombi hilo katika barua aliyomuandikia waziri mkuu Narendra Modi.
Iliandikwa
kuendana na kumbukumbu ya mwaka wa tano tangu mwanafunzi Jyoti Singh
mwenye umri wa miaka 23 alipobakwa na gengi la wanaume, kifo chake
kilichozusha maandamano ya kitaifa.
"Hakuna kilichobadilika kaika miaka mitano iliyopita," Bi Maliwal, ameiambia BBC.
"Delhi
bado ndio mji mkuu wa ubakaji. Mwezi uliopita, mtoto wa kike wa mwaka
mmoja na nusu alibakwa na gengi la wanaume, na ubakaji wa mtoto wa miaka
saba,na mwingine wa kike wa mwaka mmoja na nusu alibakwa."
Kwa wastani, alisema, watoto watatu wa kike na wanawake wasita wanabakwa katika mji mkuu huo kila siku.
India
ilifanyia mageuzi sheria zake kuhusu ubakaji kutokana na shutuma miaka
mitano iliopita, na ilichukua hatua kuharakisha kusikilizwa kesi na
kuwashinikiza maafisa wa polisi kutilia uzito tuhuma za ubakaji na
unyanyasaji wa kingono.
No comments:
Post a Comment