Watoto 10,000 wanaozaliwa Tanzania wana maambukizo ya Ukimwi
huku Watanzania 900,000 wakiendelea kutumia dawa za kufubaza makali ya ukimwi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati
akifungua majengo ya chuo cha uuguzi cha Mirembe mjini Dodoma.
Waziri Mwalimu amesema kiwango hicho ni kikubwa ambacho
kinapaswa kupunguzwa kwa juhudi za haraka kwani lengo lake ni kuona watoto wote
wanazaliwa bila maambukizo.
Wakati huo Mwalimu amekiri kuwa kiwango cha fedha
zinazotolewa na wafadhili kwa ajili ya kupambana na malaria zinatumika kwa
matangazo ambayo mengi hayana tija.
Waziri amemwagiza Katibu Mkuu kushughulikia matatizo na
mapungufu katika vyuo vya wauguzi ili viweze kutoa watu wenye ujuzi wa hali ya
juu katika kuwahudumia Watanzania.
No comments:
Post a Comment