Kiongozi wa muungano wa upinzani nchin Kenya NASA, Raila Odinga amesema yuko tayari kutumikia adhabu ya kifo baada ya kuapishwa kuwa rais wa watu.
Odinga amesema haogopi adhabu hiyo iwapo ndio itakayoleta haki ya Uchaguzi nchini Kenya.
“Namwambia Mwanasheria Mkuu kuwa tutaapishwa na kufa,” alisema Odinga huku akishangiliwa.
Kiongozi
huyo wa NASA, amesisitiza kuwa hakuna kinachomzuia kuapishwa kama rais
wa watu, lakini haijafahamika ni lini kuapishwa huko kutafanyika.
Mwanasheria
Mkuu wa serikali Githu Muigai, ameonya kuwa iwapo Odinga ataapishwa,
atakamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini, ambayo adhabu yake ni kifo
kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo.
Odinga amesema kuwa, hatambui serikali ya rais Uhuru Kenyatta pamoja na Uchaguzi wa mwezi Oktoba, uliompa ushindi.
Marekani
imemtaka Odinga kuachana na mipango hiyo na badala yake kuendelea na
harakati zake za kisiasa na kupigania haki za binadamu.
Washington DC inataka mazungumzo kati ya Odinga na Kenyatta kutatua mvutano wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment