SERIKALI ya Mkoa wa Tabora
imeziagiza Halmashauri zote kuanza upandaji wa miti ya matunda 6,000
kila moja katika Taasisi na Shule na miti isiyo ya matunda ili
kutekeleza agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akizindua awamu ya pili ya
upandaji miti kwa Wilaya ya Igunga ambapo miti 280 ilipandwa.
Mwanri alisema kuwa miti hiyo ni
sehemu ya miti milioni na laki tano (1,500,000) kwa kila Halmashauri
kila mwaka iliyoagizwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Alisema kuwa kila Halmashauri ni
lazima pamoja na kupanda miti ya aina nyingine ianze kupanda matunda
katika Shule mbalimbali na Taasisi kama vile Hospitali kwa ajili ya
kuwasaidia wanafunzi na wagonjwa.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa
kila siku anahitaji apate taarifa na takwimu kuhusu maeneo ambapo miti
imepandwa na kiwango chake kwa siku.
Aidha Mkuu wa Mkoa amewaagiza
Wakurugenzi Watendaji wote kusimamia Sheria za Mazingia ili kukabiliana
na waharibifu katika mistu mbalimbali ikiwemo wakati ovyo miti.
Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia
kurejesha uoto wa asili na viumbe wengine ambao walikwishaanza kutoweka
kutokana na uharibifu wa mistu.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa
Mkoa amewaagiza kuhakikisha wanapanga matumizi mazuri ya ardhi kwa
ajili ya shughuli za kilimo, huduma za jamii, ufugaji , mistu na
uwekezaji.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya
Igunga John Mwaipopo alisema kuwa hatamuonea huruma mtumishi au
mwananchi yoyote atakayekaidi zoezi la upandaji wa miti katika eneo
hilo.
Aliongeza kuwa hivi wanaendelea na zoezi kukamata mifugo yote inayozurura mjini na kuharibu miti na wahusika kutozwa adhabu.
No comments:
Post a Comment