
Doug Jones amakuwa mwanasiasa wa kwanza wa Democrat katika
kipindi cha miaka 25 kushinda kiti cha Seneta katika jimbo la Alabama nchini
Marekani baada ya kanpeni kali ya kumpinga mgombea wa Republican Roy Moore kwa
kura 51-49.
Huku asilimia 99 ya kura zikiwa zimehesabiwa, Bw Moore
alikataa kukubali kushindwa Jumanne usiku
Alipambana na kampeni yenye utata ambapo madai yaliibuka
kuhusu dhuluma za kimapenzi na wasichana wadogo.
Bw. Moore ambaye amesema kuwa anaamini mapenzi ya jinsia moja
yanastahili kuharamishwa amekana mara nyingi madai dhidi yake.
Vyombo vingi vya habari vimeripoti kuwa Jones ameshinda baada
ya asilimia 99 ya kura kuhesabiwa.
Lakini Moore, 70 aliwaambia wafuasi wake kuwa bado mambo
hayajakwisha.
Alisema anaamini mwanya wa ushindi utapungua wakati kura
zinaendelea kuhesabiwa.
No comments:
Post a Comment