Serikali
imewaonya viongozi wa dini wanaotumia mahubiri yao kuchambua masuala ya
kisiasa, ikiwataka kuheshimu msingi wa uanzishwaji wa taasisi zao la
sivyo taasisi zao zitafutwa.
Taarifa
iliyotolewa leo Desemba 28 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani,
Meja Jenerali mstaafu Projest Rwegasira imesema taasisi za dini
zinapaswa kuzingatia sheria na masharti ya kuanzishwa kwake ambayo yapo
kwenye Katiba za taasisi husika.
"Baadhi
ya jumuiya zimekuwa zikifanya shughuli zao kinyume na malengo yaliyomo
kwenye Katiba zao bila kuiarifu Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za kidini ya
Wizara ya Mambo ya Ndani, " amesema na kuongeza,
"Hivi
karibuni kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi wa jumuiya kutumia
mahubiri yao wakati wa ibada kuchambua masuala ya siasa kinyume na
Katiba zao. Hakuna jumuiya iliyosajiliwa chini ya sheria ya jumuiya ili
kufanya siasa."
Amesema
kufanya hivyo ni kwenda kinyume na malengo na ukiukwaji wa Kanuni ya 7
ya Kanuni za Jumuiya zilizoundwa chini ya sheria ya Jumuiya, inayotamka
pamoja na mengine kuwa Jumuiya yoyote hairuhusiwi kufanya mabadiliko ya
malengo yake bila kibali cha msajili.
“Ofisi
ya Msajili inazikumbusha Jumuiya zote kwamba ukiukaji wowote wa Sheria
ni kosa ambalo linaweza kupelekea Jumuiya husika kufutiwa usajili wake
kama ilivyoelezwa kwenye kifungu cha 17 cha Sheria husika," amesema.
Na Ibrahim Yamola, Mwananchi
No comments:
Post a Comment