Inadaiwa ugomvi huo ulitokana na kumdai
amuongeze Shilingi 4,000 kutokana na kumuuzia mabati manne chakavu kwa
jumla ya Sh. 20,000.
Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Kamishna
Msaidizi wa Polisi Jafari Mohamed, jana alithibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kumtaja mtuhumiwa kuwa ni Julius Mtoni (48) mkazi wa mjini Bunda
na watu hao walikuwa ni marafiki.
Kamanda Mohamed alisema tukio hilo
lilitokea Desema 26 majira ya mchana wakati watu hao walipokuwa
wanakunywa pombe ya kienyeji kwa mwanamke ambaye ni jirani yao.
Polisi wilayani hapa walisema Desemba
25, marehemu alimuuzia mtuhumiwa mabati manne chakavu kwa makubaliano ya
kila bati Sh. 7,000.
Walisema kuwa siku hiyo mtuhumiwa huyo
alimpatia marehemu Sh. 20,000 taslimu na kukubaliana kuwa atalipwa kiasi
kingine cha Shilingi 8,000 kilichobakia siku nyingine.
Walisema Desemba 26 wakiwa wanakunywa
pombe, marehemu alimdai mtuhukiwa amlipe Sh. 8,000 zilizokuwa zimesalia,
lakini alimpatia Sh. 4,000 ndipo wakaanza kuzozana huku marehemu
akishinikiza alipwe deni lake lote la Sh. 8,000.
Aidha, ilielezwa kutokana na
kutokuelewana, marehemu alianza kumkaba mtuhumiwa, kisha kukimbilia
nyumbani kwake na kuchukua upinde na kumfyatulia mshale ambao ulimpata
begani.
Polisi walisema kuwa baada ya marehemu
kuchomwa mshale huo aliuvunja na kubakiza kipande cha mshale huo mwilini
mwake na kukimbilia polisi, lakini alipoteza maisha kutokana na
kutokwa na damu nyingi.
“Baada ya kuchomwa mshale huo marehemu
aliuvunja na kubakiza kipande kikiwa mwilini mwake na kuja hapa polisi
kisha hospitalini, lakini taarifa ya hospitali inaeleza alikufa baada ya
kutokwa na damu nyingi,” alisema ofisa mmoja wa polisi ambaye hakuwa
tayari kutaja jina lake kwa madai sio msemaji wa jeshi hilo.
No comments:
Post a Comment