Hatua ya Pili ya michuano ya Kombe
la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup – ASFC), inaanza
rasmi kesho Jumatano Desemba 20, 2017 kwa michezo saba kuchezwa katika
viwanja tofauti.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa
na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), michezo ya kesho Desemba
20, mwaka huu itakutanisha timu za JKT Mlale y Songea na KMC ya
Kinondoni; Toto African ya Mwanza na Eleven Stars ya Kagera; Ambassador
ya Kahama na JKT Oljoro ya Manyara; Boma FC ya Mbeya na Ndanda ya
Mtwara; Mvuvumwa ya Kigoma ingawa kwa sasa imeweka maskani yake Dar es
Salaam na JKT Ruvu ya Dar es Salaam; Abajalo ya Dar es Salaam itakuwa
mwenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya wakati Milambo ya Tabora itacheza
Buseresere ya Geita.
Desemba 21, 2017 Mshikamano ya Dar
es Salaam itacheza na Polisi Tanzania ya Morogoro; Rhino ya Tabora na
Alliance ya Mwanza; Majimaji Rangeres ya Lindi itapambana na Mbeya
Kwanza ya Mbeya; Njombe Mji na Mji Mkuu ya Dodoma; Ashanti na Friends
Rangers za Dar es Salaam; Kagera Sugar na Makambako wakati Stand United
ya Shinyanga itacheza na AFC ya Arusha.
Desemba 22, mwaka huu kutakuwa na
mechi za Green Warriors na Simba; Polisi Dar itapambana na Mgambo JKT ya
Tanga; Kariakoo ya Lindi na Transit Camp ya Dar ila kwa sasa imeweka
maskani Shinyanga; Biashara ya Mara itacheza na Mawenzi Market ya
Morogoro; Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani itacheza na Madini FC
ya jijini Arusha huku Mufindi United na Pamba ya Mwanza ilihali Singida
United itacheza na Bodaboda FC.
Mchezo kati ya Simba na Green
Warriors utaochezwa Desemba 22, utakuwa ni maalumu kwa ajili ya uzinduzi
rasmi wa michuano hiyo msimu. Sababu Simba ndiye bingwa mtetezi.
Siku ya Desemba 23, mwaka huu Azam
FC itacheza na Area C; African Lyon ya Dar es Salaam na Kiluvya United
ya Pwani; Makanyagio itapambana na Mbao; Mwadui na Pepsi; Majimaji na
New Generation wakati Mbeya City itacheza na Ihefu.
Desemba 24, 2017 Young Africans
itacheza na Reha FC; Burkina ya Morogoro na Lipuli ya Iringa; Coastal
Union ya Tanga na Dodoma Fc ya Dodoma; Shupavu na Real Mojamoja wakati
Villa Squad itacheza na Mtibwa Sugar ya
No comments:
Post a Comment