Baba Mtakatifu amekutana na kuzungumza na wasanii wa Tamasha
la Krismasi mjini Vatican, tarehe 15 Desemba 2017 na kuwapongeza kwa ushiriki
huo wa Tamasha la nyimbo za “Noeli Vatican”.
Baba Mtakatifu amesema kuwa Mchango utakao patika
katika tamasha hili utawezesha kuendesha mipango kwa ajili ya watoto wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo na kwa ajili ya vijana wa Argentina.
Aidha amewasalimia wote walio andaa tukio hili, hata ambao
wataendelea na tamasha hilo Jumamosi usiku tarehe 16 Desemba 2017; pia
watakao shiriki kwa namna moja au nyingine katika kujitoa na kuenzi mahitaji ya
wenye shida, ambao wanaomba msaada na mshikamano.
“Noeli ni sikukuu inayosikika,inayoshirikisha,yenye uwezo wa
kuwasha mioyo yenye baridi, na kuondoa vizingiti vya utofauti dhidi ya jirani,
inatia moyo wa kujifungua kwa ajili ya mwingine na kujitoa bure bila kubakiza”.
Na kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anaongeza, “kuna haja leo
hii ya kuhamasisha ujumbe wa amani na undugu katika sikukuu hii ya kuzaliwa kwa
Bwana; kuna haja ya kuwakilisha tukio hili ili kuelezea hisia za kweli
zinazoihusu”.
Halikadhalika ameeleza, “kazi ya usanii ni chombo muhimu
katikati, kwa ajili ya kufungua milango ya akili na moyo kuelekea maana ya
kweli ya Noeli. Ubunifu na akili ya wasanii, na kazi zo, hata kwa muziki na
nyimbo vina uwezo wa kufikia wadau na watendaji kwa kina katika dhamiri.
Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anawatia moyo ili Tamsha la
Noeli Vatican, liweze kuwa fursa ya kupanda huruma, amani na mapokezi
yatokanayo katika Holi la Betlehemu. Na kwa kila mmoja wao anampogeza na
kuwatakia,utulivu wa Sikukuu zote za kuzaliwa kwa Bwana zenye kuwa na utajiri
wa furaha na amani. Mwisho Amewabariki!
No comments:
Post a Comment