Baba Mtakatifu
Francisko amekutana na kuzungumza na Rais wa nchi ya Bolivia mjini Vatican, Bwana Juan Evo Morales Ayma ili
kuimarisha ushirikiano na taifa hilo.
Mara baada
ya mkutano huo amekutana na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin,
akisindikizana na Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa
kimataifa mjini Vatican Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher.
Katika
mazungumzo yao wameonesha furaha kuhusu uhusiano mwema na mshikamano kati
ya Vatican na nchi hiyo hasa kwa mchango ambao Kanisa linachangia ili
kuhakikisha maendeleo ya binadamu, jamii na utamaduni wa watu wa nchi hiyo, pia
uhusiano katika Vatican na Bolivia na mada nyingine za sasa zinzohusu
pande zote mbili za nchi.
No comments:
Post a Comment