Imeelezwa kuwa zaidiya watu 2831 wameokoa kutoka 2014-2017
kupitia kituo cha kikristo cha radio cha habari maalum fm kinacho sikika ukanda wa
kasikasini mwa Tanzania.
Hayo yamesemwa na Meneja wa habari maalumfm Daniel Magulu wakati wa tathimini ya vipindi
vya radio iliyofanyika katika ofisi za habari maalum zilizopo ngaramtoni mkoani
Arusha.
Tahimini hiyo iliyo angaliwa tangau habari maalum fm ilipo
anza kurusha matangazo mwaka 2014 hadi 2017 imesema kuanzia mwaka huo watu 43 wamebatizwa.
Aidha amesema kuwa watu hao walibatizwa katika kanisa la
FPCT Habari maalum lilopo mkoani Arusha na kanisa la Hale lililopo mkoani Tanga
pia kanisa la Lake Jipe lilopo mkoani Kilimanjaro.
Hata hivyo amewataka
wakristo kuendelea kuieneza injili kwa kila mtu kama yesu kristo alivyo agiza
kuitangaza injili kwa mataifa yote
No comments:
Post a Comment