Wakati Jeshi la Polisi Tanzania kupitia
kanda maalum ya Dar es salaam likitangaza kuwa lazima litamhoji Askofu
na kiongozi wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Zachary Kakobe kwa
madai ya kutoa maneno ya kashfa kwenye mahubiri yake, wapo Wanasiasa
walioguswa na taarifa hii na mmoja wapo ni Mbunge wa Nzega Mjini Hussein
Bashe.
Kupitia akaunti ya twitter Mbunge
Hussein Bashe ameandika ;"Kesho tutazitaka Taasisi za Dini zihamasishe
amani,Maendeleo, zipongeze ni muhimu kukubali kukosolewa, Serikali
haitakiwi kufanya hivi kama hazivunji sheria.
"Taasisi za Dini zina haki ya kutoa maoni yao juu ya siasa,Uchumi na maswala yote ya kijamii, viongozi wa Dini wana nafasi yao"
No comments:
Post a Comment