Letizia Marsili, mwenye umri wa miaka 52, alitambua kwamba yuko tofauti kwa mara ya kwanza alipokuwa mdogo.
Hakuhisi
maumivu kwa haraka, jambo linalomaanisha kwamba hakuhisi alipokuwa
anateketea, au kutambua kwamba amevunjika mfupa mwilini. Jamaa zake
watano pia katika familioa yao pia walikuwa katika hali hiyo na
hawakuhisi maumivu.Letizia ameiambia BBC: "siku hata siku tunaishi maisha ya kawaida, pengine maisha bora kuliko watu wengine, kwasababu ni aghalabu sisi kuwa wagonjwa, na hatuhisia maumivu.
"Hatahivyo, ki ukweli, maumivu yapo ila ni wa sekundi chache tu."
Wanasayansi wanaamini hali hii huenda inatokana na kutofanya kazi vizuri kwa baadhi ya neva mwilini.
RWatafiti walioikagua familia hiyo wanatarajiwa kuwa uchunguzi wao utasaidia watu wanaogua mamuivu makubwa katika siku zijazo.
"Tumefungua njia mpya kwa uvumbuzi wa dawa za maumivu," amesema Prof Anna Maria Aloisi kutoka chuo kikuu cha Siena nchini Italia.
Ni kwanini wanahisi uchungu mdogo?
Kiongozi wa watafiti Dr James Cox, kutoka University College London, amesema familia hiyo zina neva mwilini, lakini "hazifanyi kazi zinavyostahili".Amesema: "TUnashughulika kupata uelewa zaidi wa kwanini hasaa hawahisi maumivu, kuona iwapo hilo litatusaidia kuvumbua dawa mpya za maumivu."
Utafiti wa wataalamu hao ambao umechapishwa katika jarida la Brain, zilishirikiana na familia kujua ni vyenzo gani vilivyounda Jini zao mwilini.
Marsili syndrome, hali hiyo iliyopewa jina la familia hiyo, inamaanisha kwamba mtu huhisi kwa kiwango kidogo mno cha joto, kuwashwana pilipili na hawahishi maumivu mifupa yao inapovunjika mwilini tofuati na watu wengine.
No comments:
Post a Comment