Shirika la anga za juu la Marekani
Nasa limegundua nyota ambayo inazungukwa na sayari nane, sawa na mfumo
wetu wa jua ambao una sayari nane.
Hiyo ndiyo idadi ya juu zaidi ya sayari kugunduiwa zikiizunguka nyota nje ya mfumo wetu wa sayari.Nyota hiyo iliyopewa jina Kepler-90, ina joto kiasi na ni kubwa kidogo kulishinda Jua.
Awali, wataalamu wa anga za juu walikuwa wamefahamu uwepo wa sayari saba pekee zilizokuwa zinaizunguka.
Lakini sasa wanasayansi wa Nasa wanasema wamegundua uwepo wa sayari nyingine ndogo iliyojaa mawe.
"Hii inaifanya Kepler-90 kuwa nyota ya kwanza kuwa na sayari nyingi sawa na za Mfumo wa Jua," anasema Christopher Shallue, mhandisi wa masuala ya programu za kompyuta katika Google, kampuni ambayo ilichangia katika ugunduzi huo.
Wahandisi kutoka kwa Google walitumia mashine yenye uwezo wa kufikiria kutafuta sayari ambazo zilikuwa awali hazionekani kwa teknolojia za awali.
No comments:
Post a Comment