Eliasa Mboma aja na Mungu kwanza Project




 


Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Eliasa Mboma  anaye tamba  na wimbo wa Shangwe anatarajia kuanzisha  Project ambayo inakwenda kwa jina la Mungu kwanza.
Eliasa  ambaye jina lake la sanaa anatambulika kama Elly From Tz ameyasema hayo katika kipindi cha Top Ten ya Habari Maalum Fm  wakati akifanya mahojiano na Muandaaji wa kipindi hicho Method Charles.
Amesema dhumuni la Project hiyo ni kuwainua  waimbaji wa Gospo Hip Hop ambao ni wachanga lakini wana hamu ya kumtukuza Mungu kupitia uimbaji wa aina hiyo.
Kwa kuanza amesema ataanza na waimbaji  Gospo Hip Hop wanne na Mmoja  atakuwa ni Muimbaji wa R&B ambao watarekodi nyimbo na kuanza  kuzisambaza kitaifa na Kimataifa baadae watakuwa na Matamasha mbalimbali kuzunguka Tanzania nzima.

No comments:

Post a Comment