Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Eliasa Mboma anaye tamba
na wimbo wa Shangwe anatarajia kuanzisha
Project ambayo inakwenda kwa jina la Mungu kwanza.
Eliasa ambaye jina
lake la sanaa anatambulika kama Elly From Tz ameyasema hayo katika kipindi cha
Top Ten ya Habari Maalum Fm wakati
akifanya mahojiano na Muandaaji wa kipindi hicho Method Charles.
Amesema dhumuni la Project hiyo ni kuwainua waimbaji wa Gospo Hip Hop ambao ni wachanga
lakini wana hamu ya kumtukuza Mungu kupitia uimbaji wa aina hiyo.
Kwa kuanza amesema ataanza na waimbaji Gospo Hip Hop wanne na Mmoja atakuwa ni Muimbaji wa R&B ambao
watarekodi nyimbo na kuanza kuzisambaza
kitaifa na Kimataifa baadae watakuwa na Matamasha mbalimbali kuzunguka Tanzania
nzima.
No comments:
Post a Comment