Kuelekeza ‘mishale’ kwenye majimbo ya ubunge yanayoshikiliwa na upinzani
ni moja ya majukumu waliyopewa washindi wa nafasi za juu katika uongozi
wa CCM wa mikoa.
Katika chaguzi hizo, waliokuwa wasimamizi, wagombea na baadaye
waliofanikiwa kushinda, wamekuwa ‘wakilishana yamini’ ya kuendesha
mkakati wa kurudisha majimbo na kata walizoshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu
wa 2015.
Lakini wakati CCM ikijipanga, Chadema imekejeli mikakati hiyo ikisema
kazi hiyo itakuwa rahisi ikiwa chama hicho kitatekeleza ahadi iliyoahidi
kwa wananchi ikiwamo kutoa Sh50 milioni kila kijiji na kutokujikita
kueneza propaganda badala ya maendeleo.
Baadhi ya mikoa inayotolewa macho na CCM ni Mbeya, Iringa, Manyara,
Arusha, Dar es Salaam ambayo upinzani ulishinda majimbo na kata nyingi
iliyowafanya kuongoza halmashauri na majiji ikiwa ni mara ya kwanza
tangu kuanza uchaguzi wa vyama vingi vya siasa mwaka 1995.
January Makamba aliyekuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa CCM
Mkoa wa Iringa aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuchagua viongozi
watakaokiwezesha chama hicho kurejesha Jimbo la Iringa Mjini
linaloshikiliwa na Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema.
“Leo tunahitimisha mchakato wa uchaguzi Iringa, tunakwenda kupata safu
mpya ya uongozi...uchaguzi ni fursa ya kupata safu mpya, kujipanga na
kujiimarisha,” alisema waziri hiyo wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais
–Muungano na Mazingira.
Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli aliongeza, “Mwaka juzi tulipata
fursa ya kuondoa vichaka hapa Iringa lakini ikashindikana, katika
uchaguzi huu ninaomba mchague kwa kuzingatia kuwa ipo haja ya kuwapata
viongozi watakaofanikisha hilo.”
Mwenyekiti mpya aliyechaguliwa, Albert Chalamila alisema chama hicho
kimepoteza mwelekeo mkoani humo kutokana na baadhi ya wanachama
kuendekeza majungu, ufitini na uongo.
Alisema jukumu lililoko mbele yake sasa ni kuwaleta pamoja wanachama ili
waweze kurejesha heshima ya chama hicho ndani ya Mkoa wa Iringa ambayo
kwa sasa imetoweka.
“Iringa leo imepoteza majimbo matatu; Iringa Mjini, Halmashauri ya
Manispaa ya Iringa na kutokana na wingi wa kura wa Chadema wakapata
mbunge wa viti maalumu… kazi iliyo mbele yetu kwa sasa ni kuhakikisha
tunarejesha majimbo hayo CCM,” alisema Chalamila.

No comments:
Post a Comment