Hakuna kitu cha msingi kiwezacho kumsaidia mtu kufanya kazi zake kwa uhuru kama kuwa na amani. Aidha katika ngazi ya mtu binafsi, kanisa, familia au Taifa. Amani ikimfunika mtu aweza kufanya mambo pasipo kuogopa nini kimezunguka mazingira aliyopo. Amani ikikosekana ndani ya moyo wa mwanadamu anapata shida sana.
Mungu mwenyewe siku zote hutuwazia mawazo ya amani katika maisha yetu ili tuishi vizuri. Maandiko yanasema ‘Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho’ #Yeremia 29:11
Ndugu yangu jifunze kuitii amani ya Mungu ndani ya moyo wako nawe hutofanya makosa mara kwa mara ambayo wakati mwingine yanaweza kukugharimu maisha yako yote yaliyo mbele yako. Mungu ni mwema hujachelewa anza sasa na Roho Mtakatifu yuko tayari kukusaidia.
No comments:
Post a Comment