Mamlaka ya Bima Tanzania Kanda ya kaskazini (TIRA) imewahimiza wazazi na walezi kuwakatia watoto  Bima ya Afya na Bima Ya Maisha ili Mtoto kusaidika pale wazazi wanapo kuwa wamekumbwa na majanga mbalimbali ikiwemo  kupoteza Maisha kwa kusomeshwa na Bima hadi Anapo hitimu elimu ya Juu.  

 

Hayo Yamesemwa na Afisa Elimu kutoka Mamlaka ya Bima Tanzania  Karo Modest mara  Baada ya Kuhitimisha  Bonanza  lililofanyika Viwanja vya Shule ya Sekondari Ilboru mkoani Arusha na Kuwa na kukutanisha Klabu za Bima kutoka Shule za Arusha Dc bonanza   lililokuwa na  lengo la kutoa elimu juu ya Umuhimu wa Bima kwa mtoto.   

 

Bonanza hilo Lilihusisha Klabu 36 kutoka shule mbalimbali zilizopo Wilaya ya Arusha Dc  huku Mwenyekiti wa Klabu na  Bonanza hilo Bi Upendo Mwakasata ambaye pia ni mwalimu Kiserian Sekondari  akibainisha kuwa   Bonanza hilo litaleta hamasa kwa Wazazi na walezi kuwakatia Bima watoto wao hususani Bima ya Maisha.

 

 
Aidha baadhi ya wanafunzi walio jitokeza kushiriki katika katika Bonanza hilo  wamesema Bonanza hilo limeleta hamsa kwa wanafunzi  na kujenga uelewa  kuhusu nini Ambacho Bima inafanya hususani kwa watoto walioko Shuleni kuanzia ngazi ya Msingi na Sekondari 

 

 
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), chini ya Sheria ya Bima Na.10 ya mwaka 2009, ni taasisi ya serikali ilioanzishwa ili kutekeleza majukumu ya kusimamia soko na kuendeleza biashara ya bima nchini na masuala yanayohusiana na bima kwa mujibu wa sheria ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

(TIRA) KANDA YA KASKAZINI YAFANYA BONANZA KUHIMIZA WAZAZI NA WALEZI KUWAKATIA WATOTO BIMA YA AFYA NA MAISHA

 

 


Serikali kupitia wizara ya kilimo Imeombwa kutengeneza sera itakayo hamasisha wakulima wa mazao mbalimbali kulima na kuhifadhi mbegu za asili ili kuzitunza zisipotee katika ramani ya Kilimo.

 

Ombi hilo limetolewa na wadau wa kilimo mkoani Arusha katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani maadhimisho yaliyo Ratibiwa na Mtandao wa Vikundi vya wakulima mkoani arusha (MVIWAARUSHA) ambayo yalifanyika  mkoani Arusha.

 

Gabriel Mwalabwi ni Mwenyekiti wa Mtandao wa vikundi vya wakulima Ekenywa amesema kuwa mbegu za asili ni mbegu ambazo zilikuwa zikitumiwa na mababu na mabibi na kwa kipindi hicho hakukuwa na Magonjwa mbalimbali ukilinganisha na hivi sasa ambapo magonjwa kwa mimea yameongezeka.

 

"Mbegu za asili tangu zamani zilivyo kuwa zikitumika zilikuwa hazina Magonjwa zinapo kuwa shambani tofauti na hivi sasa ambapo kwenye mbegu za kisasa tunaona kumekuwa na magonjwa Mengi hivyo tunaomba serikali kupitia wizara ya afya waweze kuweka sera ambayo itasaidia kulinda mbegu hizi za asili" Gabriel Mwalabwi Mwenyekiti  wa Mtandao wa Vikundi vya wakulima.


 Juliana Simon ni Mkulima kutoka mkoani Arusha ambaye amekuwa akitumia  mbegu za asili ambazo anasema kwa sehemu kubwa zimesahaulika kutunzwa huku akitolea mfano juu ya mbegu zilizo sahaulikaza Nyanya.  

 

"Zamani kulikuwa na Nyanya ndogondogo ambazo walizita nyny mshenzi lakini pia kulikuwa na nyanya ambazo zilikuwa zinajiotea na zilikuwa zina kaa muda mrefu bila kuoza tofauti na hizi sasa ambapo nyanya zinakaa muda mfupi tu zimeoza''   Alisema Juliana Saimoni Mkulima  ambaye amekuwa akitumia mbegu za asili.        


 Akitolea Majibu kuhusu utunzaji na Uhifadhi wa Mbegu za asili  kwa upande wa serikali katika maadhimisho ya siku  chakula  Duniani afisa kilimo mkoa wa Arusha Rose Moses amesema  serikali imekuwa ikiwashauli wakulima kutumia mbegu za asili kulingana na Jogrofia ya maeneo kwani kuna baadhi ya maeneo ambayo  mvua zipo chini ya wastani na mbegu.

 

Mbegu za asili ni muhimu kwa sababu zinaweza kusaidia kuendeleza kilimo cha kiasili, ambacho hakitegemei mbegu za kisasa au kemikali nyingi. Pia, zinaweza kusaidia katika kuhifadhi uhai wa mimea na viumbe vinavyotegemea mimea hiyo.

 

Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Tanzania wanafanya juhudi za kuendeleza na kuhifadhi mbegu hizi, ikiwemo kuanzisha vituo vya kuhifadhia mbegu na kutoa elimu kwa wakulima kuhusu umuhimu wa kutumia mbegu za asili.

MBEGU ZA ASILI ZILINDWE ZISIPOTEZWA NA ONGEZEKO LA MBEGU ZA KISASA : MVIWAARUSHA

 

  






Wakristo wametakiwa kumuabu Mungu katika Roho na Kweli Badala ya kuamini katika dini  kuwa  ni Mpango wa Mungu katika Kumuabudu.

 

Akihubiri katika Ibada ya Jumapili Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Naivera Church Apostolic Tanzania Lililopo Arusha  Bishop Dkt Julius Laizer amesema Kumuabudu Mungu kuna anza na Mtu ambaye Ameokoka.

 

Amesema Mkristo hawezi kumuabudu Mungu katika Roho na Kweli kama hajaokoka  kwani Yesu ndiye amepewa Mamlaka na Mungu ya Kutawala Dunia na Vitu vyote Vilivyopo ndani Yake.

 

Aidha amebainisha kuwa kuokoka sio Dini Mpya Kuokoka ni kuzaliwa mara ya Pili kwani kuzaliwa mara ya kwanza ni kile kipindi ambacho  mwanadamu anazaliwa kutoka Tumboni mwa Mama yake. 

 

Hata hivyo Sanjari na Hilo Bishop Laizer ameeleza kuwa Wokovo ni Malango wa kumfungulia Mtu  njia ya Kuanza Kumuabudu katika Roho na Kweli.


 

 CHANZO CHA HABARI

Jina : Bishop Dkt.Julius Laizer

Huduma : Naivera Church Apostolic

Mahali  : Arusha

Mamlaka : NCA

Contact : +255 74436865

 

BISHOP LAIZER : KUABUDU KATIKA ROHO NA KWELI KUNAANZA NA MTU ALIYE OKOKA