Na Method Charles
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka Himaya za Mlima Meru Mkoani Arusha Franko Titus Ayo ambaye anafanya vema na Wimbo wake Mpya ambao Unatambulika kwa Jina la Atanirejeshea amesema wimbo huo hakuutunga bali aliingia Studio na Kuanza kuimba.
Akizungumza katika Kipengele cha Gospel News kinachosikika kila siku kupitia Kipindi cha Praise Time Habari Maalum Fm Ayo amesema ni Mungu ambaye alimpa huo Wimbo Kuimba kwa ajili ya Vijana ambapo kupitia wimbo huu Vijana wengi wameokoka.
Franko Ayo ambaye ametengeneza Nyimbo zaidi ya 18 tangu amenza kuimba Muziki mwaka 2014 amebainisha kuwa aina yake ya kuimba imetengeneza kundi kubwa la Vijana kuja Kwa Yesu ukilinganisha na watu wazima.
Akijibu swali kuhusu kwanini ameimba kuwa haamini kama Mungu Yupo na kuwa Mungu anabagua katika Wimbo wake wa Atanirejeshea amesema ni Kwa sababu ya Maisha ambayo aliayapitia kiasi kwamba akahisisi Mungu hayupo na badala yake watu wanadanganya.
Ayo Alisema “Nimepitia Magumu sana Mwaka 2020 hali ambayo ilinifanya Nione kabisa hakuna Mungu lakini lilikuwa ni jambo la Muda tu kwangu na Mungu naamini Atanirejeshea”.
Aidha amebainisha kuwa anatarajia kukamilisha Albamu yake ya pili ambayo imebeba Jina la Atanirejeshea katika Mfumo wa Dvd hivyo watu wakae mkao wa kusubiri.
Hata hivyo ameomba watu kumfuatilia kupitia Channel Yake ya Yotube ambayo inakwenda kwa jina la Franko Ayo ili kuendelea Kusikiliza na Kutazama Nyimbo zake.
CHNZO CHA HABARI
FRANKO AYO
MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI
CONTACT: +25575629838
No comments:
Post a Comment