Waumuni wa Kanisa la Bunyonga, kaunti ndogo ya Kayonza wilaya Kayunga nchini Uganda ambapo mwanaume na mwanamke walikutwa wakifanya mapenzi katika madhabahu ya kanisa hilo, wamefanya ibada kanisani humo kwa mara ya kwanza baada ya kufanyiwa maombi ya utakaso.

 Kiongozi wa Kanisa hilo, Aaron Komugisha, amesema timu ya makasisi na waumini wengine kutoka Kitimbwa wakiongozwa na Kiongozi, Dan Kisitu walifanya maombi maalum katika kanisa hilo ili kulitakasa.

Waumini katika kanisa hilo waliapa kutofanya ibada kanisani hapo mpaka pale litakapotakaswa baada ya mwanaume mmoja kukutwa akifanya mapenzi na mwanamke katika kanisa hilo Jumatano iliyopita.

Wapenzi hao ambao mwanaume ni mwanandoa mwenye watoto wawili huku mwanamke akiwa ni mtalakiwa walifikishwa kwa Mwenyekiti wa kijiji, George Kanda baada ya kukamatwa wakifanya tendo hilo ambapo aliwaandikia kesi. 
 
“Tumerejesha ibada katika kanisa letu baada ya kuwa na siku ya kufunga na kufanya maombi. Sasa kanisa letu liko safi dhidi ya tendo lile la Kishetani ambalo lilifanyika,” alisema Komugisha.

Kiongozi msaidizi katika kanisa hilo, Esther Nakamate alisema,“tuanomba radhi kwa kila mtu. Tunawataka waje kanisani hapa na kuomba msamaha kwa kile walichokifanya na wasipofanya hivyo hatuwasamehe.”

IBADA ZAREJEA KANISA WALIMOKUTWA WAKIFANYA MAPENZI

No comments:

Post a Comment