Na Wena
Arusha
Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Christina Shusho awashukuru
wadau wake kwa
kumunga mkono katika wimbo wake mpya wa Relax.
Akizungumza na
radio Habari maalumu
katika kipindi cha Praise time amesema ,wimbo huo umeendelea kufanya vizuri nje na
ndani ya nchi ya Tanzania .
Shusho
ameeleza mafanikio aliyopata kupitia
wimbo huo kwamba watu
wengi wameweza kubadili mitazamo hasi na wengine kumrudia Mungu.
Aidha
amewataka wasanii wa
nyimbo za injiri kuimba
nyimbo zinazogusa maisha ya
watu na si kuimba kwa mazoea kwani
wapo wanaohitaji msaada kupitia nyimbo
Pia amewasihi
wale wote wanao pitia
changamoto hasa kiuchumi
waamini Mungu
anaweza kubadilisha maisha
yao hivyo wasiache kusikiliza
nyimbo za Injiri na Kumuomba Mungu.
Relax ni wimbo
mpya wa Christina shusho ambao
umeendelea kufanya vizuri katika station mbali mbali za radio
pamoja na Mitandao na kuwa na wasikilizaji wengi.
No comments:
Post a Comment