Wazazi na walezi wameshauriwa kutenga
muda wa kukaa pamoja na Watoto wao na kuwasikiliza ili kuwaepusha na ukatili
ambao huwaathiri kisaikolojia.
Mwezeshaji wa elimu ya afya ya uzazi na stadi za Maisha kutoka Hospitali ya Kivulini maternity Afrika Neema Donatha amewataka wazazi kuwalea watoto katika malezi bora huku wakipunguza adhabu ambazo wanazitumia kuwaadibisha.
Sambamba na hayo amewakumbusha wazazi na walezi kusimama katika nafasi zao kwa kuwa wanajukumu kubwa la kuwalinda Watoto dhidi ya ukatili.
Kwa upande wake mwezeshaji Diana Mollel amesema bado matukio ya ukatili yanaendelea kuongeza ambapo kwa shule ambazo wamezitembelea asilimia 36 wamefanyiwa ukatili wa kingono.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima amesema utafiti uliofanyika kuhusu ukatili dhidi ya watoto umeonesha asilimia 60 unafanywa na ndugu wa karibu na 40 unafanyika nje ya familia ikiwamo shuleni.
Kwa mujibu wa Takwimu za Jeshi la Polisi Tanzania kuanzia Januari hadi Desemba mwaka 2022, matukio ya ukatili dhidi ya watoto yaliyoripotiwa ni 12,163 ambapo wasichana ni 9,962 na wavulana ni 2,201 ikilinganisha na matukio ya mwaka 2021 jumla yalikuwa 11,499 ya ukatili kwa watoto yalitolewa taarifa katika vituo vya polisi.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Neema Jonathan
Huduma : Mkufunzi
Mahali : Arusha | Ngaramtoni
Kampuni : Maternity Africa
Contact : +255 752371890
No comments:
Post a Comment