Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha imetoa wito kwa Wananchi kulipa bili ya maji mapema ili kuepusha kukatiwa huduma hiyo kwa siku za usoni.
Wito huo umetolewa na afisa uhusiano kwa umma (AUWSA) Jiji la Arusha Anne Mshana wakati alipokuwa akizungumza na kituo hiki ambapo amewataka wananchi wote ambao wamejiunga na mfumo wa (AUWSA) kuzingatia ulipaji wa bili.
“(AUWSA) inatakiwa kuhudumia Jamii Zaidi na kutakiwa kuboresha huduma ya maji taka na maji safi hili halitafanikiwa kwa ufanisi endapo bili za maji Hazitalipwa Pia kutokana na matumizi yao kuna wateja wa majumbani, taasisi na Viwanda kadri wanavyo lipa kutokana na Bili zao ndivyo nasi tuvyo toa Uzalishaji unakuwa mkubwa na kuwafikia wengine ambao hawajafikiwa na huduma za maji”.
Afisa huyo ametoa ufafanuzi wa malipo ya bili za maji katika makundi yote ambayo yanahudumiwa na (AUWSA) ikiwemo taasisi na majumbani.
“Watu wa Majumbani wamegawanyika katika makundi matatu kuna watu ambao wanatumia kuanzia Unit (0) hadi (5) ambapo Unit (1) ya kwao ni sawa na Lita 1000 tasisi ni Uniti (1) ni Lita 1500 na Biashara Unit (1)ni Lita 1930 na Viwanda Unit (1) ni lita 1560”. Alisema Anne Msahana.
Naye mhandisi Ancila Temu ambaye pia ni Meneja sehemu ya usimamizi usafi wa mazingira amewataka wateja ambao wameunganishwa na huduma ya maji taka kuhakikisha hawaingizi taka ngumu kwenye kwenye mfumo huo.
“Tunawaasa watumiaji wote waliounganishiwa na wale wanao tarajia kuunganishiwa mfumo wa maji Taka ni kinyume kabisa na sheria ya Mazingira kutupa taka ambazo hazijaruhusiwa mfano pampasi za watoto na taulo za kike kutupa katika mifumo ya maji Taka kitaratibu sio sawa kama imeziba kwa mteja Tunampa adhabu Mteja Kuzibua”.
Hii ni kufuatia ripoti ya wizara maji Kuwasilishwa Bungeni Mwanzoni mwa Mwezi Mei Jijini Dodoma na Waziri Jumaa Aweso ambapo kwa sasa upatikanaji wa huduma za maji safi na salama umeongezeka kwa asilimia 88% mijini na 77% vijijini.
No comments:
Post a Comment