RAIS
Samia Suluhu Hassan amempongeza Askofu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki
Tabora, Protase Rugambwa kwa kuteuliwa na Papa Fransisco kuwa kardinali
Akitoa
pongezi hizo Rais Samia amesema, “Naungana na Watanzania wote kukutakia
kheri na kukusindikiza katika sala, unapoendelea na kazi yako ya utume
katika hatua hii mpya. Mwenyezi Mungu ambaye amekuinua kwa baraka na
jukumu hili kwenye wito wako, aendelee kukuongoza katika kulitumikia
Kanisa na jamii yetu kwa ujumla."
Pongezi hizo za Rais Samia,
zimekuja saa chache baada ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa
Fransisco kutangaza kumteua Askofu Rugambwa kuwa kardinali.
Askofu
Rugambwa na maaskofu wengine 17 kutoka Juba Sudani Kusini, Brazil,
Hong Kong, Bagota Colombia, Lisbon Ureno na Lodz Poland watasimikwa
rasmi Septemba 30, 2023
UJUMBE WA RAIS SAMIA KWA KARDINAL MTEULE RUGAMBWA
RAIS
Samia Suluhu Hassan amempongeza Askofu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki
Tabora, Protase Rugambwa kwa kuteuliwa na Papa Fransisco kuwa kardinali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment