Imeelezwa kuwa Ugonjwa wa kifafa cha mimba Husababishwa na Mama Mjamzito kuwa na ugonjwa wa kisukari.
Akizungumza na Kanzi habari Muuguzi Mkunga kutoka Maternity Africa Mariana Paul Lulu amesema kifafa cha mimba ni ugonjwa unaosababiswa na msukumo mkubwa wa damu kwa mama mjamzito.
Mariana Paul amesema ugonjwa huo hutokea mimba ikiwa na wiki (20) na baada ya mama kujifungua siku 42 huku dalili mojawapo ikitajwa kuvimba miguu na mkono.
Aidha ametaja sababu zinazopelekea mama mjamzito kupata ugomjwa wa kifafa cha mimba na kupelekea kupoteza maisha kwa mama na mtoto ni pamoja na Mama kuwa na Mwanaume zaidi ya Moja.
Baadhi ya wananchi wamesema suala la elimu kuhusu kifafa cha mimba bado haijawafikia na kuiomba serikali kuanzia nganzi ya mtaa kutoa elimu zaidi ili kujenga uelwa kwa jamii.
Kwa Mujibu wa Mfumo wa Kufuatilia vifo vitokanavyo na Uzazi (TDHS)Takwimu inaonyesha kuwa ugonjwa wa kifafa cha mimba ni ugonjwa ambao huchangia asilimia 50 na kushika nafasi ya pili kwa vifo vitokanavyo na uzazi
No comments:
Post a Comment