Wamama wanao Nyonyesha wametakiwa kunyonyesha watoto kwa Usahihili ili kumuepusha mtoto kushambuliwa na Magonjwa pindi anapo kuwa Mtumzima.

Akizungumza na Kanzi Habari Muuguzi Mkunga kutoka kituo cha Kivulini Maternity Africa LUCY JACOB amebainisha jitihada inayotakiwa kutolewa na Vituo vya afya ni kutoa elimu juu ya usahihi wa unyonyeshaji na faida za mtoto kupatiwa maziwa ya kwanza pindi Mama anapojifungua.

Aidha ameeleza madhara yatakayo tokea endapo mtoto hatanyonyeshwa vizuri kipindi akiwa mchanga ikiwa ni kupata Ugonjwa wa Manjano hali inayopelekea Kupoteza Maisha.

Sambamba na hilo baadhi ya wananchi wametoa maoni yao juu ya swala zima la unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa mtoto pindi tu anapozaliwa.

Kwa mujibu wa takwimu mpya za UNICEF kwa mwaka 2018 chini ya nusu ya watoto wote duniani au asilimia 43 ndio walioweza kunyonyeshwa katika saa ya kwanza ya uhai wao baada ya kuzaliwa hatua ambayo ni muhimu katika kumjengea mtoto kinga ya mwili na kumsaidia mama kujiweka tayari kuendelea kunyonyesha mwanaye kwa muda mrefu. 

Maziwa ya mama kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO ni zaidi ya chakula kwa mtoto, pia ni dawa ya kumkinda ma magonjwa mbalimbali na kifo.

NUSU YA WATOTO DUNIANI 50% HUNYONYESHWA MAZIWA YA KWANZA : WHO

No comments:

Post a Comment