Wakati Zaidi ya Watu Bilioni (3) Duniani wakikabiliwa na hali ya Kuto kuwa na Uhakika wa chakula na Lishe Duniani, Tanzania Imeanza kukabiliana na hali hiyo kupitia Mashirika Yasiyo kuwa ya Kiserikali yanayo jihusisha na mifumo ya kilimo na chakula endelevu kwa Kutoa Elimu kwa wanahari jinsi ya Kuripoti Taarifa hizo.
Waandishi wa Habari (20) kutoka Mkoani Arusha wamekamilisha Mafunzo ya namana bora ya Unadishi wa habari za Ikolojia na mifumo ya chakula endelevu ili kuitoa Jamii kutumia Chakula Kisicho Kuwa salama.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akihitimisha semina ya siku mbili iliyoandaliwa na wadau wa kilimo (ANSAF), (MVIWAARUSHA) na (ilesdepaix) pamoja na (FVR) Afisa program wa mitandao ya vikundi vya wakulia mkoa wa Arusha Bw.Damian Sulumo amesema mashirika haya yamekuwa wakifanya juhudi mbalimbali Za kuhamasisha wakulima kutumia mfumo wa kilimo Ikolojia.
Sulumo ametaja njia ambazo wamekuwa wakizitumia Kuhamasisha ni kupitia vyombo vya habari lengo likiwa ni kuhakikisha wanafanya uzalishaji wa chakula ambao ni endelevu na salama kwa mlaji.
Hata Hivyo Program Meneja wa shirika la (ilesdepaix) Bi.Ayesiga Buberwa amesema kuwa wao na mashirika mengine wanahamazisha kilimo cha Ikolojia kwani wanaamini kuwa ni njia bora inayosaidia kuwa na mifumo Endelevu ya chakula.
Bi.Mery Birdy ni mkurugenzi wa (OICOS) ambao wanahusika na vyakula vinavyotokana na kilimo cha ikolojia na amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuwasaisdia wakulima kujua namna ya kulima kwa kutumia mbolea ya asili na njia za asili kukinga mazao dhidi ya wadudu waharibifu.
"takribani asilimia 40 ya wakazi wa dunia, sawa na watu bilioni 3 hawana uwezo wa kupata mlo wenye afya, njaa inaongezeka halikadhalika utapiamlo na utipwatipwa,” anasema Katibu Mkuu kupitia ujumbe wake wa siku ya leo.
Inaelezwa Kuwa endapo hakuta kuwa na Jitihada za Makusudi za mifumo ya uzalishaji chakula kuanzia shambani hadi mezani kuwa na tija Zaidi na endelevu kupitia wakulima wadogo wadogo na Hata wakubwa sayari ya Dunia na watua wake itakumbwa na Uhaba wa chakula na Utapia Mlo ulio pitiliza.
No comments:
Post a Comment