Wanawake wametakiwa kupima ugonjwa wa PID mara kwa mara ili kuepuka kupata ugumba endapo watachelewa kupata huduma ya matibabu yake kwa wakati.

Hayo yamesemwa na Daktari wa magonjwa ya akina mama kutoka selian Ngaramtoni Hospital Dkt. Eliaichi Minja wakati akizungumza na Kanzihabari ya Habari Maalum fm.

Dkt. Minja amesema kuwa wanaume wengi wamekuwa wakijitibu kwa siri ugonjwa wa PID huku akijisahau kuwa anatakiwa kumtibu na mwenza wake ili kuepuka  maambukizi mapya.

Imebainishwa  kuwa ugonjwa wa PID ni maambukizi ya bakteria kwenye shingo ya uzazi,mirija ya follopio,ovari na tumbo la uzazi hasa hasa ugonjwa huo huwapata wanawake.

Dkt minja amesema kuwa zipo dalili zinazo onyesha kuwa una ugonjwa wa PID ikiwemo mwanamke kutokwa na uchafu sehemu za siri,maumivi kwenye kiuno.

Pia amesema kuna madhara yanayoweza kumpata mtu hasa katika mfumo wa uzazi ikiwemo kuziba njia ya uzazi  na mimba kutunga nje ya kizazi.

Ameongeza kuwa kuna vipimo vinavyoonyesha kuwa una ugonjwa wa PID kwa kuchukua histori ya mgonjwa,kupima Damu.

Kwa mujibu wa shirika la afya takwimu zinaonyesha kuwa Kila mwaka,zaidi ya wanawake milioni moja nchini marekani wanapatwa na ugonjwa  wa PID.

Matokeo yake zaidi ya wanawake takribani 100000 wanakuwa wagumba  kila mwaka.

Zaidi ya hayo  idadi kubwa ya mimba zaidi ya 100000 inatungiwa kwenye mirija ya uzazi inahusishwa na tatizo hilo la PID Kiwango kikubwa cha maambukizi  ni kwa wasichana wadogo.

DKT. MINJA : PID CHANZO CHA UGUMBA KWA MWANAMKE

No comments:

Post a Comment