Arusha
Naibu Makamu mkuu wa chuo Cha Nelson Mandela profesa Antony Mshandete amesema Serikali kupitia wizara ya mifugo na uvuvi imejipanga kikamilifu kuboresha Mambo yote yanayohusiana na maendeleo ya mifugo nchini.
Akizungumza
kwa niaba ya Prof. Hezroni Nonga Mkurugenzi wa huduma za mifugo kutoka
wizara ya mifugo na uvuvi, katika warsha ya program ya upimaji wa
Ugonjwa wa brusela iliyofanyika mkoani Arusha,mesema Serikali
itahahakikisha sera na miongozo inayokidhi mahitaji ya wafugaji
inawezeshwa na kuimarisha kwa maendeleo ya mifugo hususani ng'ombe wa
maziwa.
Ameongeza
kuwa Ugonjwa wa brusela ni mojawapo ya ugonjwa unaoambukizwa kwa mifugo
na binadamu ambapo wizara imetoa kipaumbele katika kuangamiza magonjwa
yanayotokana na wanyama yanayofahamika kitaalamu kwa jina la Zunosisi
ili kuendelea kuepusha maambukizi kwa mifugo na binadamu .
Kwa
upande wake mratibu wa mradi wa brusela kutoka chuo Cha Nelson Mandela
profesa Gabrieli amesema wameanzisha mradi huo ili kuzibiti ugonjwa wa
brusela katika maeneo yenye ng'ombe wa maziwa.
Hata hivyo Chuo Cha Nelson Mandela kwa kushirikia na Zoets Alfa na Wadau wengine
watawezesha programu ya upimaji wa brusela na utoaji wa vyeti kwa
wafugaji wa ngombe wa maziwa ambapo kwa majaribio wameanzaa katika
halmashauri ya meru na hai ya mkoani Kilimanjaro ili kuunga mkono
juhudi za serikali katika kukuza uchumi wa wafugaji na Taifa.
No comments:
Post a Comment