Imeelezwa kuwa Zaidi ya wagonjwa 3000 huugua  fistula kila mwaka huku wagonjwa 1300 wakipata matibabu kwa kila mwaka nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Arusha Saidi Mtanda wakati akizungumza katika Maadhimisho ya Fistula Mkoani Arusha nchini Tanzania.

Mtanda amesema  Kwa Mujibu wa Utafiti Ulio fanywa na UNFPA takwimu zinaonyesha Wagonjwa wanao pata matibabu ni 1300 kati ya wagonjwa 3000 wanao kumbwa na ugonjwa huo .

"Mtakubaliana na mimi kuwa taifa letu limepiga hatua kubwa kutokomeza magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa fistula, hapa kivulini wameeleza kwamba wanawake kwa maelfu wanaishi na ugonjwa huu na kwa Mujibu wa shirika la UNFPA nchini Tanzania hivi sasa kuna wanawake kati ya 10000 hadi 20000 wanao ugua Fistula" Alisema Mtanda

Akizungumza kuhusu Ugonjwa huo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya akinamama Katika Kituo cha Kivulini maternity Africa Kinacho jihusisha na Utoaji wa Tiba kwa Wagonjwa wafistula Kanda ya Kaskazini amesema Fistula ni ugonjwa unao Tibika Wamama wanao ugua ugonjwa huu wajitokeza kwani matibabu ni Bure.

"Fistula ni ugonjwa ambao husababisha shimo kati ya uke na kibofu cha mkojo au njia ya haja kubwa na uke, husababishwa na mama kukaa na uchungu wa muda mrefu bila kujifungua" Alisema Dr. Fedrick Mbise

Lucy Mollel ni Afisa Rasilimali watu Kutoka Kivukini Maternity Afrika amebainisha kuwa Zaidi ya wagonjwa 400 wametibiwa katika kituo cha Afya Kivulini Tangu Kituo hicho kimeanzishwa  huku wakirajia kuwafikia wagonjwa 150 wa fistula kwa kila mwaka.

Takwimu za UNFPA zinakadiria kwamba takriban wanawake milioni 2 Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara, Asia, ulimwengu wa Kiarabu, Amerika Kusini na Caribbea wanaishi na Fistula na visa vipya kati ya 50,000 hadi 100,000 hutokea kila mwaka duniani kote.

Shirika la afya duniani WHO linasema tatizo hilo la Fistula linaweza kuepekwa kwa wasichana kuchelewa kupata mimba ya kwanza, kwa kuachana na mila potofu kama ukeketaji, na kupata huduma za afya ya uzazi.

Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Fistula Duniani ni  Tokomeza Fistula Wekeza kwenye afya Bora wezesha Jamii.

TAFITI : WAGONJWA 3000 HUGUA FISTULA KILA MWAKA TANZANIA

No comments:

Post a Comment