RAIS Samia leo Jumanne Februari 22, 2022 amesema hana tabia ya kutukuzwa wala kulinganishwa na Mungu na kwamba atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu wa kusikiliza maoni ya wengine.
Rais Samia amesema hayo katika sherehe za Jubilee ya miaka yake 25 inayofanyika wilayani Ngara mkoani Kagera.
Alikuwa akijibu kauli iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi aliyeemuomba Rais Samia kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile.
“Baba Askofu katika kufunga hotuba yako umeniasa mambo ya kukataa
kutukuzwa na mimi nataka nikuahidi mbele ya umma huu kwamba, hii si
tabia yangu na ninajitahidi kujishusha niwe sawa na wengine. Maana
utumishi huu kama mipango ya Mungu ilivyo ameniweka hapa niwatumikie na
siyo nijitukuze kwenu kwahiyo nitawatumikia,” amesema Rais Samia.
No comments:
Post a Comment