MADIWANI VITI MAALUM ARUMERU MAGHARIBI WAZIFUATA KERO MASHINANI KULETA UWAJIBIKAJI NA KUZITATUA

 


Madiwani wa Viti maalum Jimbo la Arumeru Magharibi, wamewataka Wanawake Kutoa Ushirikiano na Kuwa tayari katika utekelezaji wa Zoezi la sensa na Makazi kwa mwaka 2022 hatua ambayo itasaidia serikali katika Kutoa Huduma zinazo Stahili katika Maeneo Yao.

 

Wakiwa katika Ziara ya Kutembelea Miradi Mbalimbali Katika Jimbo la Arumeru Magharibi Kijiji cha Lemanyata Wamesema Katika Kaya Mama ni Mtu Sahihi kutoa Takwimu sahihi ili Kusaidia Serikali Kupanga Bajeti kwa Usahihi.

 

“Tujitoe katika Kutoa Ushirikiano katika Zoezi ambalo Lipo Mbele Yetu la Sensa ya Watu na Makazi Sisi Ni watu Sahihi wanawake ndio Viongozi wa Kaya, Kila mKazi atambulike Nyumba kwa Nyumba na Watakuja wataalamu Kwaajili ya zoezi Hilo” Alisema Grace Seneu Diwani wa Ololieni.

 

Wakiwa Katika Kijiji cha Lengijave walifanikiwa Kukutana na wamama ambao Wamenufaika katika Mikopo ya Vikundi.

 

Afisa maendeleo Wa Kijiji Hicho Amesema Wamama Wamekuwa wakishindwa Kuunda Kwa Sababu ya Kutaka Mikopo Binafsi na siyo ya Vikundi.

 

“Elimu Tunatoa kuhusu Mikopo ya Halmashauri lakini Watu wanapenda Mikopo Ya Chapuchapu na Watu wanapenda Mikopo Binafsi na siyo ya Vikundi”Agripina Chuwa Afisa Maendeleo Kijiji cha Lengijave.

 


      Picha ya Pamoja Ya Baadhi ya Madiwani Katika Ziara Jimbo la Arumeru Magharibi

Katika Ziara Hiyo Wamebaini Changamoto ya Kuto kuwa na Mtalaamu wa Maabara hali ambayo Inafanya Wagonjwa kushindwa kupata Vipimo Sahihi katika Kituo Cha Afya cha Olkokora.

 

Edna James Maeda Muuguzi katika Kituo cha Afya Olkokola amesema Changamoto Nyingine ni Kukosekana kwa usafiri Kutoka Katika Kituo hicho cha afya hadi Hospital ya Wilaya Hasa kwa wamama wajawazito wanapo pata Tatizo la Kujifungua.

 

“Changamoto ni Usafiri Mama Mjamzito anapo pata Matatizo Hakuna Chumba cha Upasuaji”Alisema Edna Maeda Muuguzi Kituo cha Afya  Olkokola.

 

Diwani wa Kiutu Nina Pama Amewataka Wamama Kuhakikisha kutunza Mazingira kwa Kupanda  Miti Hasa wakati Huu ambapo Mvua Zinanyesha.

 

Mwenyekiti wa Madiwani Elinipa Laizer amebainisha  Kuwa atatatua Changamoto hizo Kwa Kufikisha Sehemu Husika Ili ziweze Kutatuliwa kwa wakati.

 

Ziara Hiyo yenye lengo la kubaini kero na changamoto zinazo wakabili  wananchi wa Arumeru Magharibi  Madiwani walioshiriki ni Madiwani kutoka Tarafa mbalimbali  akiwemo Elinipa Laizer kutoka Lemanyata, Nina Masanja Kutoka Kiutu, Aneth Kifwe Kutoka Elboru na Grace seneu Kutoka Olorien.

 

 Madiwani wa Viti Maalum wengine walio Kuwa katika Ziara Hiyo ni Araf Said kutoka Bangata, Stella Ephraim Kutoka Kimnyaki, Faraja Emmanuel Kutoka Oltrument, Happy Thomas Kutoka Oltrument na  Muna Jama Kutoka Mukrat.

 

 

 

No comments:

Post a Comment