Mwimbaji Wa Nyimbo Za Injili Kutoka Ukanda Wa Kaskazini Imani Mwasambapa Ambaye Pia Kitaaluma Ni Daktari Ametoa Wimbo Mpya Uitwao SWEET JESUS.
Akizungumza Na Gospel Climax Ya Habari Maalum Media amesema Anatarajia Kufanya Tamasha Kubwa La Kusifu Na Kuabudu Mungu Na Jijini Arusha Tanzania.
“Mwaka Huu Tutakuwa Na Event Moja Live Praise And Worship Concert Ambayo Itafanyika Jijini Arusha Wote Mnakaribishwa Tumuabudu Mungu”Amesema Imani Mwasambapa.
Aidha Amesema Kuwa Wimbo Huo Mpya Ambao Ameutoa Kwa Jina La SWEET JESUS Upo Tayari Utakua Unapatikana Kwenye Channel Yake Ya Youtube Huku Maandalizi Mengine Yakiendelea Kufanyika Ili Uweze Kuonekana Na Kila Mtu.
“Kwasasa Wimbo Wa Sweet Jesus Utapatikana Youtube Na Boomplay, Na Collection Za Nyimbo Zangu Zote Zitapatikana Pale”Amesema Imani Mwasambamaba.
Vile Vile Mwimbaji Mwasambapa Amesema Kuwa Anapokea Mialiko Mbalimbali Kila Anapopewa Mualiko Itategemea Na Vile Ambavyo Mungu Atamuongoza Kufanya Maana Sio Kila Mualiko Kuupa Kipawambele Bali Kumshirikisha Mungu.
“Mialiko Hii Yakawaida Huwa Nafanya Mungu Akinipa Nafasi Ya Kwenda Kufanya Huwa Naenda Kwasababu Sio Kila Kilichopo Unatakiwa Wewe Ufanye Hapana Kwasababu Mungu Anatoa Kwa Nafasi Kwahio Mungu Akitoa Nafasi Ninakwenda”Amesema Imani Mwasambapa.
Hata Hivyo Amewashukuru Wadau Wake Wote Ambao Wanasikiliza Nyimbo Zake Na Kumshika Mkono Kwa Njia Moja Ama Nyingine.
Dkt Imani Mwasambapa Amewahi kufanya Kazina Waimbaji Mbalimbali Akiwemo Beda Andrew na Wengine Wengi kama Mwalimu wa Kwaya.
CHANZO CHA
HABARI
Jina : Dkt Imani Mwasambapa
Huduma : Mwimbaji
Contact : +255655652130
No comments:
Post a Comment