Watumishi wa Mungu wametakiwa kumtumikia Mungu Kama ambavyo Mungu amewaita ili Mungu aweze kuwatumia katika Viwango alivyo Kusudia.
Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Moriah Pentecote lililopo Ngusero Mkoani Arusha Bishop Elibariki Mmbando wakati Akisimika Viongozi Wapya katika kanisa hilo.
Bishop Mmbando amebainisha kuwa kiongozi wa Kiroho hatumiki kwa faida zake Mwenyewe Bali anatumika kwa faida za Mungu ambaye amemuweka katika Uongozi.
“Mungu anapo Mwita Mtu anaweka ndani yake Maono na Maono hayawezi kutimilizwa na Mtu Mmoja hivyo kanisa linahitaji watu wa kufanya kazi pamoja tatizo katika Kanisa la Leo watu wanapo itwa na Mungu Kupitia watumishi hawamtumikii Mungu kama walivyo itwa na Mungu na badala yake wamekuwa wakifanya kinyume na Kuua Kanisa”.
Aidha amebainisha kuwa endapo Watumishi ndani ya Kanisa watafanya kazi kama walivyo Itwa, Mungu atawatumia Katika Viwango alivyo Kusudia na kufanya Kanisa Kustawi na Kukua.
No comments:
Post a Comment