Jumapili ya tar 14 ya mwezi huu wa kumi na 11 kanisa la mahali la FPCT kurasini chini ya Mchungaji Kiongozi David Batenzi ambaye ni Askofu Mkuu Mstaafu FPCT ameongoza ibada ya kutangazawa Tawi la Mbagala Zakmem kuwa Parishi na Mchungaji John Jilangila kubarikiwa kuwa Mchungaji wa Parishi.
Zakhem inakuwa parishi ikiwa na jumla ya matawi manne ambayo ni Zakhem yenyewe ,tawi la Kizuiani, tawi la Tuangoma na tawi la Vianzi, lakini pia kuna kanzi mpya mbili ambazo ziko chini ya Zakhem ambazo ni Mfulumwambao na Funza maeneo ya Mbagala.
Askofu Batenzi akihubiri katika ibada hiyo amesisitiza wachungaji na washirika kuifanya kazi ya Mungu kwa juhudi na kuhakikisha wanaifikia jamii inayowazunguka kwa Injili na kufungua makanisa mengi inavyowezekana.
Kwa upande wake Mchungaji John Jilangila ambaye ndio Mchungaji wa Parishi hiyo mpya anamshukuru Mungu kwa kuwa Parishi na kushukuru kanisa la mahali kurasini kuwaamini na kuwapa kuwa Parishi.
No comments:
Post a Comment