WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI MHANDISI KAMWELWE, AMUAGIGA KATIBU MKUU WA WIZARA HIYO KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA YA KIUTENDAJI KWENYE BOHARI KUU YA MAJI



 


NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAZIRI
wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Issack Kamwelwe, amesitisha manunuzi yote ya
vifaa vya maji yanayofanywa na Bohari Kuu ya Maji jijini Dar es Salaam hadi
hapo Serikali itakavyoelekeza vinginevyo.
Lakini
pia ameagiza mamlaka zote zinazotekeleza miradi ya maji au zinazoendesha utoaji
wa huduma ya maji waende bohari kuu kuangalia vifaa vinavyoweza kutumika kwao
ili wavinunue viishe kabla ya kuelekea kwenye hatua nyingine.
Kumekuwepo
na ununuzi holela wa vifaa Halmashauri na Mamlaka za maji zimekuwa
zikijinunulia vifaa jinsi wanavyotaka nah ii ni hatari sana ndio maana miradi
mingi haiendani na thamani halisi ya vifaa, na vinapatikana kwa gharama kubwa
mnno, Aalisema Mhandisi Kamwelwe.
“Mamlaka
zote za maji zilizo chini ya wizara yangu, mtu asije akaenda kununua vifaa nje
ya bohari kuu kama kifaa hicho kinapatikana kwenye bohari hiyo.” Alisema
Mhandisi Kamwelwe.
Na
kumuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji
kwenye bohari hiyo kwani kwa hali ilivyo imeshindwa kabisa kutekeleza majukumu
yake.
Mheshimiwa
Waziri alitoa maagizo hayo wakati alipotembelea bohari hiyo iliyoko Boko jijini
Dar es Salaam, mwanzoni mwa ziara yake ya kutembelea miradi ya maji
inayotekelezwa na Serikali kupitia DAWASA Desemba 5, 2017.
Alilaumu
utendaji duni wa watendaji wa Bohari hiyo unaoonyesha kuishiwa ubunifu. Na hivyo
kufanya shughuli kulegalega.
“Serikali
imenunua vifaa vyenye thamani ya shilingi bilioni 4.83 vingine vinaonekana vimepitwa
na wakati, lakini vingine vinaonekana vinaweza kutumika, na boharia inahitaji
watu ambaom ni wabunifu, na kwa vile vilivyopitwa na wakati viko viwanda
vinatengeneza vifaa kama hivyo uongozi ni bora ukawasiliana na viwanda hivyo
ili waone tatizo ni nini na inawezekana kuboresha eneo ambalo linavifanya
visitumike ili vikaweza kutumika na kuokoa fedha za serikali.
“Nakuagiza
ufanye kazi hiyo kwa haraka na umpatie taarifa Katibu Mkuu, sitaki kuona kitu
hata kimoja kinapotea kwani vifaa hivi vimenunuliwa na kode za wananchi na
fedha za serikali.” Aliagiza Waziri Kamwelwe.
Katika
hatua nyingine, Waziri amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kufanya
mabadiliko makubwa ya kiutendaji kwenye bohari hiyo ili pawepo na wataalamu
husika kuloingana na shughuli za bohari.

Aidha Waziri ametoa muda wa mwezi mmoja kwa wadeni wote wa Bohari Kuu ya Maji, kulipa madeni yao vinbginevyo atachukua hatua baada ya muda huo kupita.

No comments:

Post a Comment