Dodoma
Mbunge wa Mtambwe (ACT Wazalendo), Khalifa Mohamed Issa ameitaka Serikali kueleza iwapo iko tayari kukaa meza moja na watu wanaojitangaza kuwa na uwezo wa kuwafufua watu waliokufa.
“Je Serikali ni lini itakaa pamoja na watu wanaosema kuwa wana uwezo wa kuwafufua watu waliokufa, ili waweza kuwarudisha wapendwa wetu waliofariki dunia,” Khalifa.
Katika swali la nyongeza Mbunge huyo amehoji ni waganga wangapi wanaopiga ramli chonganishi wamekamatwa na kuchukuliwa hatua hadi sasa.
Akijibu Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamza Hamis amesema operesheni na misako ya mara kwa mara imekuwa ikifanyika kuwakamata waganga wanaopiga ramli chonganishi na manabii wa uongo wanaodanganya na kuwatapeli wananchi.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri, katika kipindi cha mwaka 2020 wapiga ramli chonganishi 57 walikamatwa na kufikishwa mahakamani na kwamba kesi zao zipo katika hatua mbalimbali.
No comments:
Post a Comment