Arusha
Mwimbaji Wa Nyimbo Za Injili Nchini Tanzania Florida Thomas Ambaye Kitaluma Ni Therapist Amesema Kuwa Hajawahi Kuulizwa Na Paroko Wake Kuhusu Kusimama Kama Mwimbaji Binafsi.
Akizungumza Katika Kipindi Cha Top Ten Ya Habari Maalum Fm Kinacho Sikika Kila Jumamosi Saa Kumi Na Moja Kamili Jioni Hadi Saa Moja Kamili Usiku Amesema Romani Katoliki Na Kuimba Nyimbo Binfsi Sio Kosa.
Florida Amesema Anasali Katika Kanisa La Sinoni Parokia Ya Mtakatifu Ambrose Kibuka Na Paroko Wa Kanisa Hilo Ni Father Henry Sawelo.
Amesema Padri Sawelo Akiwa Kiongozi Wake Wa Kiroho Hajawahi Kumuuliza Kuhusu Kuimba Binafsi (Solo Artist) Badala Ya Kwaya Kama Ambavyo Imekuwa Kawaida Ya Kanisa La Roman Katoliki Na Amesema Sio Dhambi.
“Hajawahi Nilaumu Mbali Na Kunishauri Jinsi Ya Kufanya Vizuri Katika Imani Na Pia Nimekuwa Na Mwalimu Wa Kwaya Wa Kanisa La Sinoni Parokia Ya Mtakatifu Ambrose Kibuka Ambaye Amekuwa Msaada Mkubwa Katika Kutunga Nyimbo”Alisema Florida Thomas Mwimbaji Wa Nyimbo Za Injili Nchini Tanzania.
Pia Kwa Upande Wa Kwaya Ya Kanisani Amesema Kuwa Wamekuwa Wakimchukulia Ni Mwimbaji Pasipo Na Shaka Na Wamekuwa Wakimsaidia Anapo Hitaji Msaada Na Amekuwa Akishiriki Katika Shughuli Za Kwaya Yake Pia.
Hata Hivyo Ametaja Changamoto Ambayo Amewahi Kukukutana Nayo Ikiwemo Kurekodi Albamu Yake Ambayo Ilibidi Arekodi Sehemu Mbili Baada Ya Kazi Yake Ya Mwanzo Kufutika Mkoani Dodoma Na Baadae Kuja Kurekodi Huku Mkoani Arusha.
Waimbaji Ambao Ni Roman Katoliki Ambao Wamekuwa Wakiimba Nyimbo Binafsi Tofauti Na Kwaya Kama Ambavyo Imezoeleka Kwa Kanisa La Roman Ni Pamoja Na Rebeka Malope Kutoka Afrika Kusini Na Nchini Tanzania Ni Upendo Shayo Kutoka Arusha.
Florida Thomas Ni Mwimbaji Wa Nyimbo Za Injili Lakini Kitaalamu Ni Therapist Aliyepata Degree Yake Afrika Kusini Na Baadae Kurejea Nchini Tanzania Kufanya Kazi Hiyo.
Chanzo Cha Habari
Jina : Florida Thomas
Huduma : Mwimbaji Wa Nyimbo Za Injili
Mahali : Arusha
Kanisa : Roman Catholic Parokia Ya Sinoni
No comments:
Post a Comment