Mirerani.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Zephania Chaula Alhamisi Machi 25, 2021 ataongoza wananchi kumuombea mapumziko mema aliyekuwa Rais wa Tanzania marehemu, John Magufuli.
Akizungumza Jumatano Machi 24, 2021 katibu tawala wilayani humo, Zuwena Omary amesema shughuli hiyo itafanyika kati mji wa Mirerani.
Omary amesema mbali na Chaula, watakuwepo viongozi mbalimbali wa dini na kwamba wakazi wa mji huo na maeneo jirani watashiriki.
Mkazi wa Mirerani, Sokota Mbuya amesema atamkumbuka Magufuli kwa kufanikisha udhibiti wa madini ya Tanzanite yasitoroshwe kwa kujenga ukuta unaozunguka migodi ya madini hayo.
"Hivi sasa husikii tena India na Kenya kuongoza kwa mauzo ya madini ya Tanzanite zaidi ya nchi yetu ya Tanzania na kodi inalipwa kutokana na ukuta uliojengwa na Magufuli," amesema Mbuya.
No comments:
Post a Comment